Wafuasi Wa Kasisi Ezekiel Wakusanyika Nje Ya Mahakama wakitaka Aachiliwe

zaidi ya watu 110 wamefukuliwa katika Msitu wa Shakahola, Pwani ya kenya na mwinjilisti huyo maafufu amehusishwa pakubwa na maafa hayo

0

Kumeshuhudiwa kizaazaa nje ya Mahakama ya Shanzu mumbao wa pwani ya Kenya,Mombasa leo hii Jumanne, Mei 2, baada ya mamia ya wafuasi wa Mchungaji Ezekiel Odero kukusanyika katika mahakama hiyo.

Kasisi Ezekiel anafikishwa kortini leo ambao anashtakiwa na makosa ya mauaji ya halaiki. aidha Ezekiel Atafahamu iwapo ombi lake la kauachiliwa kwa dhamana litakubaliwa. polisi vile vile wameiomba mahakama hiyo kuwapa muda wa siku 30 ya kuendelea kumzuilia mchungaji huyo wakati uchunguzi ukiendelea.

Wakiongozwa na msaidizi wake ambaye pia ni kakake Mchungaji Gillack Odero, walipinga kukamatwa kwake kwa kuomba aachiliwe.

Kasisi Ezekiel Odero na kasisi Paul Mackenzie wanatarajiwa kufika mbele ya mahakama ya Shanzu leo hii kwa mashtaka ya itikadi kali, ugaidi, mauaji ya halaiki na utakatishaji fedha.

zaidi ya watu 110 wamefukuliwa katika Msitu wa Shakahola, Pwani ya kenya na mwinjilisti huyo maafufu amehusishwa pakubwa na maafa hayo

Gillack alionekana akiamuru umati mkubwa wa watu wakati akiwaongoza katika kuimba, huku mara kwa mara wakiwasihi maafisa wa polisi kuachilia Ezekiel.

Mnamo Jumapili, Gillack aliwahakikishia wafuasi wa Ezekiel kuwa watulivu akionyesha imani kwamba kanisa la kasisi huyo lililokumbwa na utata eneo la Mavueni, Kaunti ya Kilifi, litafunguliwa tena hivi karibuni.

Wafuasi wa Ezekiel wakiomba nje ya mahakama ya Shanzu

Ezekiel alikamatwa Alhamisi, Aprili 27, baada ya Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuanza kufuatilia uhusiano wake na Mauaji ya Shakahola.

Mara tu baada ya kukamatwa, Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki alitangaza kwamba mwinjilisti huyo maarufu atashtakiwa kwa mauaji ya halaiki ya watu

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted