Azam TV Kupeperusha Mubashara Mechi za Ligi Kuu Ya Kenya

Kampuni ya Utangazaji ya Tanzania Azam TV wametia saini FKF za haki za utangazaji wenye thamani ya KES 8 milioni.

0

Shirikisho la Soka la Kenya FKF na Kampuni ya Utangazaji ya Tanzania Azam TV wametia saini mkataba wa wiki moja wa haki za utangazaji wenye thamani ya KES 8 milioni.

Hii inamaanisha kila klabu kati ya 18 ya Ligi Kuu ya Kenya itapokea ksh 300,000 kwa sababu haki za TV ni za klabu zote za ligi kuu ya FKF.

Ksh 2 milioni zilizosalia zitatumika kulipia malimbikizo ya marupurupu ya wasimamizi wa mechi.

“Tunafuraha kutangaza kwamba shirikisho limepata mkataba wa muda mfupi wa udhamini wa utangazaji na Azam Media Limited kwa awamu ya 30 ya FKF PL.

‘’Kama sehemu ya makubaliano, Azam Sports itarusha FKF-PL mechi ya raundi ya 30 kati Kariobangi Sharks FC na Tusker FC ambayo  imeratibiwa kuchezwa Mei 13, 2023 katika Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo na mechi ya raundi ya 30 ya FKF-PL nambari. 269. kupokea KES 300,000 kama sehemu ya mpango huo” Ilisema FKF

Vilabu pia vimeombwa kulipatia Shirikisho akaunti zao za benki zinazotumika kabla ya tarehe 12 Mei 2023.

“Vilabu vinaombwa kuthibitisha maelezo yao ya benki, kwa maandishi kupitia nyaraka iliyotiwa saini kabla ya Ijumaa Mei 12, 2023, ili kuwezesha malipo ya fedha hizo,” iliongeza FKF

Kwa mujibu wa mkataba huo, Azam TV itarusha moja kwa moja mechi 2 za Ligi Kuu ya Kenya FKF wikendi hii:

Kariobangi Sharks dhidi ya Tusker FC Uwanja wa Nyayo Jumamosi na Mashemeji Derby, Gor Mahia dhidi ya AFC Leopards Jumapili kutoka Uwanja wa kimataifa wa  Nyayo

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted