Yanga Yatwaa Ubingwa Wa Ligi Kuu Bara Kwa Mara Ya 29

Yanga yatawazwa mabingwa wa ligi kuu Bara kwa mara ya pili mtawalia. Yanga imetetea ubingwa wake baada ya kuishinda Dodoma Jiji magoli 4-2

0

Yanga yatawazwa mabingwa wa ligi kuu Bara kwa mara ya pili mtawalia. Yanga imetetea ubingwa wake baada ya kuishinda Dodoma Jiji magoli 4-2 katika mechi ya kusisimua iliyopigwa ndani ya uwanja wa Azam Complex Jijini Dar es Salaam

Yanga  imefikisha pointi 74 ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yoyote huku pia ikibakiwa na michezo miwili ambayo ni dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons.

Ubingwa huu kwa Yanga ni wa 29 kwake kuuchukua tangu mwaka 1965 ikiwa ndio vinara ikifuatiwa na Simba iliochukua mara 22.

Bao la Musonda linamfanya nyota huyo kufikisha mabao mawili ya Ligi Kuu Bara hadi sasa baada ya awali kufunga katika ushindi wa mabao 3-1, dhidi ya Geita Gold, Machi 12, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Tangu Dodoma Jiji ipande Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/2020 haijawahi kuifunga Yanga kwani katika michezo sita waliyokutana baina yao imepoteza mitano na kuambulia sare mmoja tu.

Hii ni ushindi wa pili wa yanga baada ya kuishinda wapinzani wao simba katika kombe la community shiled  msimu ulipokuwa ukiaza mwezi agosti tarehe 13 2022.

Yanga bado wanawania kombe la shilikisho barani Africa. Kwa sasa wako mguu mmoja ndani ya fainali ya kombe hile baada ya kuizaba Marumo Gallants magoli 2 katika awamu ya kwaza jijini Dar es salaam . Yanga watakuwa wakielekea Africa kusini kucheza na Marumo katika awamu ya pili tarehe 17 mwezi huu. Iwapio Yanga itatwaa ushindi, basi watakuwa wakumenyana katika fainali hiyo dhidi ya mshindi kati ya ASEC Mimosas na USM Alger ya Algeria.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted