Mbio za WRC Safari Rally Kenya Yapata Ufadhili

Kampuni Ya, Bang Bet imetangaza kuwa itafadhili madereva wawili wa Mbio Za safari Rally, Gerald Maina, na John Ngugi Katika awamu ya  mwaka huu la Mashindano ya Ubingwa...

0

Kampuni Ya, Bang Bet imetangaza kuwa itafadhili madereva wawili wa Mbio Za safari Rally, Gerald Maina, na John Ngugi Katika awamu ya  mwaka huu la Mashindano ya Ubingwa wa Dunia (WRC) ya safari rally yatakayofanyika Kaunti ya Nakuru kati ya tarehe 22 na Tarehe 25 Juni 2023.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bang Bet Leonardo Varese alisema lengo kuu la ufadhii huu ni kuhakikisha wanaboresha na kukuza talanta kwa wapenzi wa safari rally.

‘’ Huu ni mchezo wa gharama kubwa. Kwa hivyo tunatafuta watu ambao wana hari na hamu ya kuendesha gari na labda hawana rasilimali kamili ya kutosha na wanahitaji kuongezwa kupigwa jeki kidogo. Kwa hivyo hawa jamaa (Gerald na John) wameomesha uelediwao na kwa hivyotumewaweka katika mpango wetu’’.  Alisema Bw. Leonardo

Dereva was safari rally bwana John Ngugi alitoa shukrani zake kwa Kampuni hiyo akisema anatumai kuwa na safari njema wakati mashindano ya safari rally ya WRC litakaporejea wiki Ijayo.

‘’ Mchezo huu wa safari Rally ni ghali sana. Kwa hivyo tunawashukuru sana Bangbet kwa kutukabidhi chapa yao. Letu ni kuwaonyesha kuwa tuko tayari kwa kazi hiyo’’ Alisema Ngugi

Ngugi atashiriki mbio hizo akitumia gari la Subaru Impreza N16 iliyokuwa inamilikiwa na Don Smith. Awali alikuwa akitumia gali la Mitsubishi Evo 9

Maina, kwa upande mwingine, atakuwa akiendesha Mitsubishi Evo 9 na atashiriki kwa Mara ya Kwanza kwenye Mashindano ya Safari tangu kurejeshwa kwenye kalenda ya WRC.

‘’Tangu BangBet ilipokuja, tulianza maandalizi yetu kwa sababu hatukuwa na matumaini ya kupata mfadhili mapema. Kwa hivyo tulifurahi walipokuja wakisema watatupatia ufadhili. Kusema kweli, tuna furaha sana’’. Alisema Maina

Hili litakuwa awamu  70 ya Mashindano ya Dunia ya safari Rally.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted