Madonna aahirisha ziara baada ya kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi

Kulingana na meneja wake, maambukizi ya mwanamuziki huyo wa kimataifa yalikuwa "mabaya" na yalisababisha "kukaa kwa siku kadhaa katika chumba cha ICU". Aliongeza kuwa afueni kamili inatarajiwa.

0

Mwanamuziki Madonna ameahirisha ziara yake ya kimataifa baada ya kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) akiwa na maambukizi makali ya bakteria.

Kulingana na meneja wake, maambukizi ya mwanamuziki huyo wa kimataifa yalikuwa “mabaya” na yalisababisha “kukaa kwa siku kadhaa katika chumba cha ICU”. Aliongeza kuwa afueni kamili inatarajiwa.

Katika taarifa yake, Guy Oseary alisema afya ya Madonna inaendelea kuimarika, lakini bado yuko chini ya uangalizi wa kimatibabu. Madonna anaaminika kupokea matibabu katika hospitali moja huko New York City, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti.

Mwanamuziki huyo nyota wa pop alitarajia kusherehekea kumbukumbu ya miaka 40 ya wimbo wake mpya, Holiday, kwa kuanza ziara yake ya kwanza ya vibao bora zaidi. Ziara iliyopewa jina la ‘Celebration Tour’, ingekuwa ni kurejea kwa mwimbaji huyo baada ya maonyesho yake ya majaribio ya Madame X mnamo 2019 na 2020.

Baadhi ya maonyesho hayo yalisitishwa kwa sababu ya majeraha ya goti na nyonga. “Samahani ilibidi niahirishe usiku wa leo,” nyota huyo aliandika kwenye Instagram baada ya kughairi onyesho la 2020 huko Lisbon, “lakini lazima nijisikize mwili wangu na kupumzika!” Ziara ya hivi punde zaidi ya Madonna ilipaswa kuanza Vancouver, Canada, tarehe 15 Julai na kumalizika tarehe 30 Januari huko Mexico City.

Lakini meneja wa mwimbaji-mtunzi huyo wa nyimbo alisema Madonna alipata “maambukizi makubwa ya bakteria” Jumamosi 24 Juni na matokeo yake, ahadi zote zitahitaji kusitishwa. Alitarajiwa kuanza ziara yake huko Uingereza na Ulaya kidogo tarehe 14 Oktoba, iliyopangwa kuanza na kumalizika huko O2 Arena, London.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted