Vyama vya Afrika Kusini vyatia saini mkataba wa kukiondoa chama tawala cha ANC

Muungano wa vyama saba vya kisiasa nchini Afrika Kusini umetia saini mkataba wa kutaka kukiondoa chama tawala cha African National Congress (ANC) katika uchaguzi wa 2024. Mkataba wa...

0

Muungano wa vyama saba vya kisiasa nchini Afrika Kusini umetia saini mkataba wa kutaka kukiondoa chama tawala cha African National Congress (ANC) katika uchaguzi wa 2024.

Mkataba wa Vyama vingi vya Afrika Kusini ulisema iwapo wataingia madarakani, watafanya kazi pamoja na kutenga nyadhifa za mawaziri na ubunge.

Pia wanalenga kukizuia chama cha Economic Freedom Fighters cha Julius Malema kupigiwa kura kuingia madarakani.

Makubaliano hayo yanakuja wakati nchi hiyo ikikabiliana na hali mbaya ya uchumi, ufisadi, ukosefu wa ajira na mzozo wa nishati.

Wachambuzi wanasema ANC iko hatarini kupoteza wingi wake wa wabunge kwa mara ya kwanza tangu Afrika Kusini irejee kwenye demokrasia mwaka 1994.

Kambi hiyo mpya, hata hivyo, haijaamua ni nani atachaguliwa kuwa rais ikiwa itafaulu katika uchaguzi huo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted