Jeshi: Ali Bongo Yuko ”Huru Kufanya Anachotaka”

Rais wa mpito wa Gabon Jenerali  Brice Oligui sasa ametangaza Ali Bongo yuko 'huru' na anaweza kuondoka nchini. Jenerali  Oligui amesema hayo katika taarifa kwa vyombo vya habari...

0

Rais wa mpito wa Gabon Jenerali  Brice Oligui sasa ametangaza Ali Bongo yuko ‘huru’ na anaweza kuondoka nchini. Jenerali  Oligui amesema hayo katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyosomwa moja kwa moja Jumatano jioni kwenye runinga ya taifa.

‘’Ali Bongo Ondimba, yuko “huru kufanya anachokitaka” na “anaweza kwenda nje ya nchi, ikiwa anataka,” Kanali Ulrich Manfoumbi Manfoumbi ametangaza kwenye televisheni ya serikali, akisoma taarifa kwa vyombo vya habari “iliyotiwa saini” na Jenerali Oligui, ambaye sasa anaongoza taifa hilo.

Ali Bongo, amekuwa madarakani kwa miaka 14, alikuwa chini ya kizuizi cha nyumbani tangu mapinduzi ya kijeshi ya Agosti 30, yaliyotekelezwa bila umwagaji damu chini ya saa moja baada ya kambi yake kutangaza kuchaguliwa kwake tena katika kura iliyoelezwa kuwa ya udanganyifu na viongozi wa mapinduzi.

“Kwa kuzingatia hali yake ya afya, aliyekuwa Rais wa Jamhuri Ali Bongo Ondimba yuko huru kufanya anachotaka. Anaweza, akipenda, kwenda nje ya nchi kufanya uchunguzi wake wa afya,” taarifa hiyo kwa vyombo vya habari imeongeza.

Ali Bongo alipatwa na kiharusi kibaya mnamo mwezi Oktoba 2018 ambacho kilimfanya adhoofike kimwili, huku mguu wake wa kulia na mkono hasa akivitumia kwa shida.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted