Watu Zaidi Ya 2,100 Waangamia Katika Tetemeko La Ardhi Morocco

Tetemeko hilo ni baya zaidi kuwahi kutokea Morocco tangu lile la mwaka 1960 lililouharibu vibaya mji wa Agadir na kusababisha vifo vya watu 12,000.

0
People carry the remains of a victim of the deadly 6.8-magnitude September 8 earthquake, in the village of Imi N’Tala near Amizmiz in central Morocco on September 10, 2023. – Using heavy equipment and even their bare hands, rescuers in Morocco on September 10 stepped up efforts to find survivors of a devastating earthquake that killed more than 2,100 people and flattened villages. (Photo by FADEL SENNA / AFP)

Morocco inaomboleza vifo vya zaidi ya watu 2100 vilivyosababishwa na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea Ijumaa usiku.

Wafanyakazi wa dharura kutoka nje ya Morocco sasa wamejiunga na juhudi za uokoaji, usaidizi unaohitajika sana, kwani kila saa inayopita inapunguza uwezekano wa kupata manusura.Wanajeshi na wafanyakazi wa kutoa misaada wameonekana wakipeleka maji na mahitaji mengine katika vijiji vilivyoathiriwa.

Janga hilo, hadi sasa limesababisha takribani watu wengine wasiopungua 2,000 kujeruhiwa wengi wao wakiwa katika hali mbaya kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni huku idadi hiyo na ya vifo ikitarajiwa kuendelea kuongezeka.

A woman reacts by the rubble of destroyed buildings in the aftermath of the deadly 6.8-magnitude September 8 earthquake, in the village of Imi N’Tala near Amizmiz in central Morocco on September 10, 2023. – Using heavy equipment and even their bare hands, rescuers in Morocco on September 10 stepped up efforts to find survivors of a devastating earthquake that killed more than 2,100 people and flattened villages. (Photo by FADEL SENNA / AFP)

Tetemeko hilo la ardhi lenye ukubwa wa 6.8 kwa kipimo cha Richter lilitokea umbali wa kilomita 72 kusini magharibi mwa mji wa kitalii na wakihistoria wa Marrakech ambapo liliviharibu vijiji vingi. Familia nyingi katika mji wa Marrakech zimelala nje kwa usiku wa pili baada ya mkasa huo zikihofia kuwa nyumba zao hazina tena usalama.

Mamlaka nchini humo zimetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa. Rabat imekubali misaada kutoka Uhispania, Uingereza, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Ufaransa, Marekani na baadhi ya nchi nyingine wanasema wako tayari kusaidia. Uhispania imetuma waokoaji 86 katika timu mbili, na mbwa wanne wa kunusa.

Tetemeko hilo ni baya zaidi kuwahi kutokea Morocco tangu lile la mwaka 1960 lililouharibu vibaya mji wa Agadir na kusababisha vifo vya watu 12,000 ambao walikuwa theluthi moja ya idadi jumla ya watu mjini hapo kwa wakati huo.

Timu ya taifa ya ya soka ya Morocco liliongoza shughuli za utoaji damu kwa waathiriwa wa mkasa huo. mchuano kati ya morocco na Liberia ya kufuzu kwa kombe la mataifa bara la Afrika pia lilifutiliwa mbali ili kuomboleza na familia zilizoathirika

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted