Wanasoka Wa Kimataifa Wa Libya Ni Miongoni Mwa Walioangamia Katika Mafuriko

Mafuriko makubwa Jijini Derna, Nchini Libya yameangamiza maisha ya wachezaji soka kadhaa wa hali ya kiwango cha kimataifa.

0

Mafuriko makubwa Jijini Derna, Nchini Libya yameangamiza maisha ya wachezaji soka kadhaa wa hali ya kiwango cha kimataifa. Haya ni kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Libya, LFF.

Mafuriko hayo yalisababishwa na Kimbunga Daniel na ilikuwa kwa kasi mno na kusababisha mabwawa mawili kuvuja kingo zake, na kusomba sehemu kubwa ya mji wa bandari wa mashariki wa Derna.

Meya wa Derna anakadiria kuwa watu 20,000 wanahofiwa kuuawa huku Maelfu ya watu bado wanaripotiwa kupotea.

LFF imetangaza rasmi vifo vya wanasoka wanne katika eneo hilo ambao ni Shaheen Al-Jamil, Monder Sadaqa na kaka wawili Saleh na Ayoub Sasi.

Sadaqa aliichezea Darnes inayoshiriki Ligi Kuu ya Derna, ambapo ndugu wa Sasi walikuwa sehemu ya timu ya vijana.Al-Jamil hivi majuzi alisajiliwa na Al-Tahadi, timu nyingine ya Ligi Kuu katika jiji la Benghazi.

Mwanasoka Ibrahim Al-Qaziri, pia alifariki katika mafuriko hayo. Alikuwa amechezea timu kadhaa za Ligi Kuu ya Libya na hivi karibuni alikuwa Nusour Martouba wa daraja la pili.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted