Timu Ya Raga Ya Kenya Yatwaa Ubingwa Wa Afrika Na kufuzu Kwa Michezo Ya Olimpiki 2024

Timu ya raga ya Kenya, Shujaa wamefuzu kwa Michezo yao ya Olimpiki baada ya kuishinda Afrika Kusini 17-12 katika fainali ya Kombe la Africa Rugby 7s

0

Timu ya raga ya Kenya, Shujaa wamefuzu kwa Michezo yao ya Olimpiki kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuishinda Afrika Kusini 17-12 katika fainali ya Kombe la Africa Rugby 7s kwenye Uwanja wa Harare Sports Club mjini Harare, Zimbabwe Jumapili Septemba 17, 2023.

Ilikuwa fainali ya kukata na shoka ambayo iliifanya Shujaa kustahimili shinikizo kali la mapema lkutoka kwa Blitzboks ya Afrika Kusini. Hata hivyo Patrick odongo aliweza kuwakwepa na kufunga Try  kisha Tonny Omondi  akasawazisha Conversion yake na kufanya mambo kuwa 7-0.

Shujaa walipambana hadi kuwalemea Afrika kusini na kutwaa ubingwa wa Afrika.

Kikosi hicho kinachonolewa Kevin Wambua kilistahimihili mashambulizi ya Blitzboks  kadiri muda ulivyosonga hadi kipenga cha mwisho kilipopilizwa. Michezo ya Olimpiki 2024 yatafanyika jijini Paris, Ufaransa Mwezi Julai

Shujaa walielekeza ushindi  kwa marehemu mamake Patrick Odongo aliyeaga jumamosi iliyopita. Odongo alikuwa Nguzo Muhimu katika ushindi wa Shujaa. Alifunga Try 7 na pia kutawazwa mchezaji bora wa mchezo huo

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted