Chadema Yaanza Mchakato Mzima Kuelekea Uchaguzi Mkuu

CHADEMA, Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe kimepata uongozi mpya kwa ajili ya kuongoza Chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ambapo kimeahidi kuwaunganisha wanachama na wananchi ambao ndio...

0

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe kimepata uongozi mpya kwa ajili ya kuongoza Chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ambapo kimeahidi kuwaunganisha wanachama na wananchi ambao ndio chanzo cha nguvu ya umma.

Uchaguzi wa Viongozi wa CHADEMA Jimbo la uchaguzi Vwawa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe umefanyika mjini Vwawa na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Wilaya, Mkoa na Kanda ya Nyasa.

Alitangaza matokeo ya uchaguzi, Msimamizi wa Uchaguzi huo katika Jimbo la Vwawa Songwe Aneth Chonya ambaye ni Katibu mstaafu wa CHADEMA Jimbo la Urambo Tabora, pamoja na nafasi nyingine amemtangaza Mchungaji Amoni Tuloline Mwashitete kuwa mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Vwawa akishinda kwa kura 130 dhidi ya Ephraim Amoni Mwakateba aliyepata kura 25 huku Katibu mwenezi akiibuka Selemani Mgalla.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Mch. Amoni Mwashitete, amewashukuru wajumbe kwa kumuamini pamoja na wenzake na kuahidi ushirikiano ili kwa pamoja wakalipe deni kwa kukitumikia Chama hicho ambacho ni cha wanachama.

Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Songwe Isakwisa Lupembe amewahimiza Viongozi na wanachama kukijenga Chama chao hicho kwa kufanya kazi kwa umoja na kuepuka unafiki ndani na nje ya Chama na kuheshimu katiba na miongozo ya ngazi za juu za CHADEMA.

Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Gwamaka Mbughi amewataka Viongozi wa CHADEMA kuendelea kufanya kazi kwa weledi na uaminifu ili kuendelea kuwa tumaini la wananchi katika kuongoza Taifa la Tanzania wakijiandaa na chaguzi zijazo.

Frank Mwakajoka ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wagombea Kanda ya Nyasa na ndiye alikuwa Mbunge wa Tunduma pamoja na Mwenyekiti wa BAWACHA Mkoa wa Songwe Agness Chilulumo wamezungumza kwenye Mkutano huo mkuu wa Uchaguzi

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted