Taifa Stars Yaapa Kufa Na DR Congo

Timu ya taifa stars ya Tanzania itashuka dimbani usiku wa leo dhidi ya Vijana kutoka DR congo katika mchuano wa kufa mtu ambayo Tanzania lazima washinde ili kufuzu...

0
Tanzania’s forward #10 Mbwana Samatta (L) fights for the ball with Zambia’s midfielder #17 Clatous Chama (C) during the Africa Cup of Nations (CAN) 2024 group F football match between Zambia and Tanzania at Stade Laurent Pokou in San Pedro on January 21, 2024. (Photo by SIA KAMBOU / AFP)

Timu ya taifa stars ya Tanzania itashuka dimbani usiku wa leo dhidi ya Vijana kutoka DR Congo katika mchuano wa kufa mtu ambayo Tanzania lazima washinde ili kufuzu raundi ya 16 bora ya muondoano.

Kindumbwendumbwe hicho cha kukata na shoka litaanza saa tano uiku saa za afrika mashariki. Kwa sasa Taifa stars inavuta mkia katika kundi F na alama moja baada ya kutandikwa mechi ya ufunguzi dhidi ya Morocco na kutoa sare ya moja kwa moja na Zambia.

Tanzania’s forward #12 Simon Msuva controls the ball during the Africa Cup of Nations (CAN) 2024 group F football match between Zambia and Tanzania at Stade Laurent Pokou in San Pedro on January 21, 2024. (Photo by SIA KAMBOU / AFP)

Matokeo hayo yalisbabisha kucha mkuu Adel Amrouche kutimuliwa kazi kwa kuwa pia alikuwa na adhabu ya nidhamu kutoka kwa shirikisho la soka barani Africa CAF

Tangu michuano ya afcon iasisiwe, Tanzania haijawai shinda mchuoano wowote wa kombe la bara Africa na macho yote sasa hususan Africa mashariki itakuwa ikiangazia majirini wao iwapo wataondoa kinaitwa na wengi kama laana.

Katika mashindano ya afcon ya mwaka huu baadhi ya mataifa yenye uzoefu wa mashinado hayo wamebwagwa na mataifa yenye historia ndogo ya afcon. Equatorial Guinea waliifunga wenyeji ivory Coast magoli mane kwa nunge na kuiacha the elephant hatarini ya kuyaaga mashindano hayo.

Mauritania’s midfielder #8 Bodda Mouhsine holds a Mauritania flag after his team won the Africa Cup of Nations (CAN) 2024 group D football match between Mauritania and Algeria at Stade de la Paix in Bouake on January 23, 2024. (Photo by KENZO TRIBOUILLARD / AFP)

  Kwa upande mwingine Mauritania walipata ushindi wao wa kwanza katika mashindano hayo dhidi ya miamba wa soka afrika, Algeria. Ushindi wa Mauritania uliwawezesha kufuzu raundi ya muondoano.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted