Raila Akatiza Kampeni zake za Uenyekiti AU Kutetea Madaktari Wanaogoma Kenya

Kiongozi huyo wa ODM ameitaka Serikali kuwalipa wahudumu wa matibabu, kuangalia ada na mishahara ya madaktari wanaoendelea na masomo zaidi na kushughulikia kusitishwa kwa huduma zao bila utaratibu.

0

Takriban mwezi mmoja tangu madaktari kote nchini Kenya waanze mgomo wao, kiongozi wa Upinzani Raila Odinga kwa Mara ya kwanza amekatiza kampeni zake za kutafuta kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika AU ili kuangazia mzozo huo akitaka serikali kushughulikia mkwamo huo.

(Photo by SIMON MAINA / AFP)

Huku akiulizwa maswali na wasiwasi kutoka kwa baadhi ya Wakenya waliohoji ukimya wake kuhusu suala hilo, kiongozi huyo wa ODM alisema Wakenya wameteseka vya kutosha kwa sababu ya mzozo huo. Odinga alisema kuwa mgomo huo umetatiza huduma za afya katika hospitali za umma nchini.

“Tuna wasiwasi kwamba hali inazidi kuwa mbaya na hivi karibuni, tutakuwa na shida kamili ambayo wafanyikazi wote wa afya watapunguza zana zao. Tayari maafisa wa kliniki wamejiunga,” alisema.

Raila alitoa wito kwa serikali na madaktari kujadiliana pamoja kuhusu masuala yaliyoibuliwa na kuepusha mateso zaidi kwa Wakenya.

“Baada ya mashauriano mapana, nina imani kuwa madaktari na wahudumu wengine wote wa afya walio kwenye mgomo kwa sasa wataweza kutengeneza mpango wa kurejea kazini na kuanza kazi tena ikiwa serikali itatimiza matakwa yao nusu wakati mazungumzo yakiendelea,” alisema Raila .

Kiongozi huyo wa ODM ameitaka Serikali kuwalipa wahudumu wa matibabu, kuangalia ada na mishahara ya madaktari wanaoendelea na masomo zaidi na kushughulikia kusitishwa kwa huduma zao bila utaratibu.

By AFP)

Raila  pia alitoa wito kwa serikali kurejesha malipo ya KSh206,000 kwa wanafunzi wanaofanya kazi hadi pale mazungumzo ya CBA yatakapofanyika.

Mgomo wa madaktari umeingia siku ya 24 leo huku wahudumu wa kliniki, mahabara na wa lishe wakijiunga no katika mgomo.

By AFP

Hata hivyo, serikali yakenya kupitia wizara ya Usalama imetangaza mgomo huo kuwa haramu na kuwapa wahudumu hao afya masaa 48 kurejea kazini la sivyo watachukuliwa hatua za kisheria.

(Photo by SIMON MAINA / AFP)

Wiki iliyopita rais wa Kenya William Ruto alitangaza serikali haina pesa ya kuwalipa madaktari na kuwasihi kuwa wangwana na kurejea karini mara moja.

Photo by SIMON MAINA / AFP)

Kunti kadha imetangaza kuwafuta kazi baadhi ya wahudumu na kuwajiri wengine kwa muda.  Licha ya hayo yote madaktari wamesimama kidete kuwa mgomo wao utaendelea hadi serikali itemize matakwa yao ya nyong’eza ya mishahara na mazingira bora ya kufanya kazi.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted