Rais Ruto amteuwa mkuu mpya wa majeshi ya Ulinzi Kenya

Kabla ya Uteuzi wake, jenerali Kahariri alikuwa naibu Mkuu wa majeshi ya ulinzi Kenya

0

Rais wa Jamhuri ya Kenya William Samoei Ruto amempandisha cheo Charles Muriu Kahariri hadi kiwango cha Jenerali na kumteua kuwa mkuu mpya wa majeshi ya Kenya KDF.

Kabla ya Uteuzi wake, jenerali Kahariri alikuwa naibu Mkuu wa majeshi ya ulinzi Kenya. Kuteuliwa kwa Jenerali Kharairi umetokana na kifo cha aliyekuwa mkuu wa  majeshi ya Ulinzi Jenerali Francis Ogolla.

Jenerali Ogolla alifariki wiki mbili iliyopita kufuatia ajali mbaya ya Ndege.

Meja jenerali John Mugaravai Omenda amepandishwa cheo na kuwa Lieutenant General na kuteuliwa kuwa naibu mkuu wa majeshi ya Ulinzi ya Kenya.

Kabla ya uteuzi wa leo, Jenerali Omenda alikuwa akihudumu kama kamanda wa jeshi la wanahewa.

Meja Jenerali Fatuma Gaiti Ahmed amehamishiwa jeshi la wanahewa na kuteuliwa  kamanda  mkuu wa jeshi la wanahewa

Fatuma Gaiti anakuwa mwanamke wa kwanza Kenya kuteuliwa wadhifa huo wa kamada wa jeshi la wanahewa

Rais William Ruto vile vile amemteua  Meja Jenerali Paul Owuor Otieno kuwakamada wa  jeshi la wanamaji

Chuo kikuu cha ulinzi nchini Kenya kimepata naibu chansela mpya kwa jina meja jenerali Thomas Njoroge Ng’ang’a ambaye atahusika na masuala ya usimamizi na fedha.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted