Tahadhari ya Kimbunga Hidaya yatolewa Kenya na Tanzania

"Huenda Kenya ikakabiliwa na kimbunga cha kwanza kabisa

0

Rais William Ruto amesema huenda Kenya ikakabiliwa na kimbunga chake cha kwanza kabisa. Akizungumza wakati wa hotuba yake kwa taifa la Kenya Ijumaa katika Ikulu ya Nairobi, Ruto amesema Kimbunga Hidaya kinaweza kupiga wakati wowote. Ruto alisema Idara ya Hali ya Hewa ya Kenya na IGAD, imetoa onyo kali kwa wanancnhi

Ruto alisema nchi lazima ichukue hatua haraka na kwa uamuzi ili kupunguza athari mbaya za mzozo uliopo na kulinda maisha na mali.

“Kimbunga hiki, kwa jina Hidaya, kinaweza kupiga wakati wowote na kinatabiriwa kusababisha mvua kubwa, upepo mkali na mawimbi makali na hatari ambayo inaweza kutatiza shughuli za baharini katika Bahari ya Hindi na makazi katika pwani ya Kenya,” alisema.

“Nchi yetu lazima ichukue hatua madhubuti na haraka ili kupunguza athari mbaya za mzozo uliopo na kulinda maisha na mali.”

Nchini Tanzania Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa ya mwenendo wa kimbunga “HIDAYA” kilichopo katika Bahari ya Hindi mashariki mwa pwani ya nchi mwa Tanzania

‘’Kimbunga HIDAYA kimeendelea kuimarika na kusogea kuelekea maeneo ya pwani ya nchi yetu ambapo hadi kufika saa tatu asubuhi ya tarehe 03 Mei 2024 kilikuwa umbali wa takriban Kilomita 342 Mashariki mwa pwani ya Mtwara,’’ TMA imesema.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted