East Africa Natural disasters Tanzania

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania yatangaza uwepo wa kimbunga Dikeledi

Kwa sasa, kimbunga hicho hakiashirii uwezekano wa kusababisha athari za moja kwa moja hapa nchini. Hata hivyo, kutokana na ukaribu wa maeneo ambayo kimbunga “DIKELEDI” kipo sambamba na maeneo ya kusini mwa nchi yetu, upo uwezekano mdogo wa matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa katika maeneo ya Pwani ya kusini hususan katika Mikoa ya Lindi na Mtwara kwa siku ya leo tarehe 14 ya Januari, 2025.