Katekista adaiwa kumbaka mwanafunzi wa kidato cha tatu mkoani Njombe
Simon Njavike (43) mkazi wa Mlangali wilayani Ludewa, mkoani Njombe, ambaye ni katekista wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mlangali amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya wilaya hiyo akidaiwa kumbaka mwanafunzi wa kidato cha tatu mwenye umri wa miaka 17.