Kesi ya Kabendera dhidi ya Vodacom anayoituhumu kuhusu kutekwa kwake kusikilizwa leo
Katika kesi hiyo Kabendera anaoimba mahakama hiyo iiamuru kampuni hiyo imlipe fidia ya Dola za Marekani 10 milioni ambazo ni sawa na shilingi bilioni 28, akiituhumu kuwa ndio iliyofanikishwa kukamatwa kwake na askari Polisi, tukio analoliita kutekwa, na kisha kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi, mwaka 2019.