Waziri Mkuu Kassim Majaliwa azindua kamati ya kitaifa ya AFCON 2027
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 05, 2024 amezindua Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) na kuahidi kuwa Serikali itafanya nayo kazi kwa karibu ili iweze kufanikisha malengo ya Tanzania kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.