Shahidi: Wanachama wa Chadema Wananitishia mimi Kuja Kutoa Ushahidi
Shahidi huyo alidai kuwa kuna wanachama au wafuasi wa CHADEMA wanaofahamu kuwa anakuja kutoa ushahidi na kwamba walimtishia kwa kumwambia kuwa “lolote baya linaweza kumkuta.”
All news and updates from Tanzania
Shahidi huyo alidai kuwa kuna wanachama au wafuasi wa CHADEMA wanaofahamu kuwa anakuja kutoa ushahidi na kwamba walimtishia kwa kumwambia kuwa “lolote baya linaweza kumkuta.”
Shahidi huyo alisisitiza kuwa kwa ufahamu wake kuzuia uchaguzi ni kosa.Aidha, alipoulizwa kuhusu shtaka la Uhaini linalomkabili Lissu, shahidi alisema anafahamu Lissu anashtakiwa kwa Uhaini lakini alikiri hafahamu vipengele vyote vya shtaka hilo zaidi ya madai ya kauli zinazohusiana na uchaguzi.
Shahidi huyo mkazi wa Arusha mwenye umri wa miaka 26 amekiri kutokuwepo kwa baadhi ya maelezo ya ushahidi wake ambapo katika ushahidi aliousema Mahakamani leo, baadhi ya maelezo hakuandika katika maelezo yake ya Polisi.
Shahidi wa 10 wa Jamhuri ameieleza Mahakama sababu zilizomfanya kutoa ushahidi wake akiwa kwenye kizimba cha siri, akidai kuwa anahofia usalama wa maisha yake.
Shahidi alidai kuwa Aprili 3, 2025 alikuwa katika doria jijini Arusha akiwa na askari wengine wanane, wakitumia gari aina ya Toyota. Wakiwa doria, alipokea maelekezo kupitia *radio call* kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha, Boni Mgogo, kuhusu taarifa za vijana wanaodaiwa kuhamasishana kuzuia Uchaguzi Mkuu wa 2025 katika eneo la Mromboo
Shahidi alidai kauli hiyo ilimpa hamasa ya kuwahamasisha vijana wenzake wa mtaani zoezi ambalo alilifanya Aprili 8, 2025 katika eneo la Njoro maarufu Pepsi.Hata hivyo wakati akiendelea na zoezi hilo kuwahamasisha ghafla alikamatwa na Polisi huku wenzake wakikimbia
Shahidi huyo alipoulizwa namna alivyobadilika kutoka kuwa mtuhumiwa wa kupanga maandamano yasiyo na kibali hadi kuwa shahidi katika kesi ya uhaini, P6 alijibu kuwa hafahamu.
Shahidi huyo, mwenye umri wa miaka 33 na mkazi wa Kibangu, wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam, aliiambia Mahakama kuwa anajishughulisha na biashara ndogondogo ya kuuza viatu na soksi katika maeneo ya Mchikichini, Feri na Posta Mpya. Pia hufanya kazi ya kuosha magari mara kwa mara.
Lissu alipinga muundo wa kizimba hicho akieleza kuwa kinazuia hata majaji kumuona shahidi na kufuatilia mienendo na tabia zake wakati wa kutoa ushahidi, jambo alilodai linakiuka kanuni ya tatu ya ulinzi wa mashahidi.
The case has been postponed to Wednesday, 11th 2026.