Politics Tanzania

Nape ajiondoa kwenye mtandao wa X(Twitter) baada ya kutumbuliwa Uwaziri.

Itakumbukwa kuwa taarifa ya Ikulu ya utenguzi wa Nape ilimkuta Waziri huyo wa zamani akiwa katikati ya hafla ya utoaji tuzo za wanawake wa kidigitali zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam ambako alikuwa mgeni rasmi. Shughuli hiyo ilikuwa ikirushwa mubashara na kituo cha televisheni cha TV E. iliyotumwa kati ya majira ya saa mbili usiku na saa tatu.