Uganda: Waandamanaji wanaopinga mfumuko wa bei wafyatuliwa vitoza machozi
Polisi nchini Uganda waliwarushia gesi ya kutoa machozi waandamanaji waliokuwa wakiandamana kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta na vyakula vya msingi
Polisi nchini Uganda waliwarushia gesi ya kutoa machozi waandamanaji waliokuwa wakiandamana kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta na vyakula vya msingi
Macron anatazamiwa kufanya mazungumzo Jumanne asubuhi katika ikulu ya rais na mwenzake Paul Biya, 89, ambaye ametawala Cameroon kwa takriban miaka 40.
Somalia ilitangaza kupiga marufuku mirungi kutoka Kenya mnamo Machi 2020 huku kukiwa na mzozo wa mpaka wa baharini kati ya majirani hao wawili wa Afrika Mashariki.
Mohamed Adel alipatikana na hatia mwezi uliopita kwa ‘mauaji ya kukusudia’ ya Nayera Ashraf, mwanafunzi mwenzake wa chuo kikuu ambaye alikataa kuwa katika uhusiano nae.
Kundi la M23 ‘March 23 Movement’ lilipata umaarufu wakati liliteka kwa muda mji wa Goma mashariki mwa Congo mwaka 2012 kabla ya kufurushwa katika mashambulizi ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na Congo.
Odinga, 77, waziri mkuu wa zamani na Naibu Rais William Ruto, 55, ndio wagombea wakuu katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9.
Tume Huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) imelaani kukamatwa kwa maafisa watatu kutoka kwa kampuni inayosambaza mifumo ya kielektroniki ya kupigia kura kwa uchaguzi wa mwezi ujao.
Matangazo mengi ya nafasi za ajira zina dalili zinazofanana: zina makataa mafupi, huahidi mishahara mikubwa na mara nyingi hujumuisha kiungo kwenye jukwaa la nje la mtandao linaloomba maelezo ya kibinafsi.
Kujiuzulu kwa Draghi kumekuja baada ya vyama kadhaa muhimu katika muungano wake vuguvugu lenye nguvu la 5-Star, chama kikubwa zaidi katika serikali ya mseto ya nchi hiyo, kususia kura ya imani