Nchi sita zaitaka Madagascar kufanya mazungumzo na waandamanaji
Kisiwa hicho cha Bahari ya Hindi kilikuwa kinangoja uteuzi wa waziri mkuu mpya baada ya Rais Andry Rajoelina kuvunja baraza lake lote la mawaziri Jumatatu, hatua aliyochukua kutuliza maandamano yaliyoshika kasi tangu Septemba 25 kutokana na malalamiko ya uongozi mbaya pamoja na ukosefu wa maji na umeme.