Tshisekedi: Jeshi linatekeleza wajibu wake dhidi ya uvamizi wa M23
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Felix Tshisekedi, amesema jeshi lake linatekeleza wajibu dhidi ya wapiganaji wanaoungwa mkono na Rwanda, waliovamia maeneo mapya mashariki mwa nchi, na alionya juu ya uwezekano wa “kuongezeka kwa mivutano” katika eneo hilo.