Search
Close this search box.
Africa
Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti CCM(Bara)

Halmashauri kuu ya CCM imepitisha kwa kauli moja jina la aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Abdulrahman Kinana kuwa Makamu mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara.

Kikao hicho kilichoketi chini ya mwenyekiti wake Samia Suluhu Hassan kimempitisha Kinana kuchukua nafasi ya Philip Mangula ambaye leo ameandika barua ya kuachia nafasi hiyo

Jina la kinana litapitishwa na wajumbe wa Mkutano mkuu maalum unaotarajiwa kufanyika April Mosi, katika ukumbi wa Jakaya Kikwete uliopo Mkoani Dodoma

Wakati huohuo, Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana hii leo mkoani Dodoma imemsamehe aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje nchini Tanzania Benard Membe na kumrejeshea uanachama kuanzia hii leo.

Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje nchini Tanzania, Benard Membe

Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM itikadi na uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema, msamaha huo ni kwa mujibu wa Ibara ya 48 kifungu cha 8 cha katiba ya CCM na kwamba wamezingatia maombi ya barua zake za kuomba msamaha kwa chama

Alipoulizwa kama ameomba kurudishiwa uanachama, Shaka amesema, Membe amewahi kuandika barua mara tatu kuomba kurejeshewa uanachama wake na sasa NEC imeamua kumrejeshea hadhi hiyo aliyoondolewa tangu mwaka 2018

Mbali na Membe, NEC pia imemrejeshea uanachama Abdallah Maulid diwani ambaye amewahi kuwa muwakilishi wa jimbo la Jang’ombe ambaye nae aliondolewa hadhi hiyo sambamba na Membe mwaka 2018

Comments are closed