Search
Close this search box.
Africa

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewaua watu watatu wanaodaiwa kuwa majambazi waliokuwa katika mpango wa kupora katika duka moja la miamala ya fedha eneo la Mbagala Zakhiem jijini Das res Salaam. 

Akizungumza na wanahabari hii leo Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Jummanne Muliro amesema kuwa tukio hilo lilitokea jana na watu hao wanaodaiwa kuwa majambazi walikuwa wakitumia usafiri wa  pikipiki na baada ya kugundua kuwa wanafuatiliwa na polisi walianza kurusha risasi.

“Baada ya kuanza kurusha Polisi walijihami kwa kutumia silaha ambapo waliwajeruhi na baada ya kufikishwa hospitali waligundua kuwa wameshapoteza maisha, Uchunguzi umebaini kuwa mtandao wao bado unaendelea,” amesema Muliro.

Amesema baada ya ukaguzi walibaini kuwa watu hao walikuwa na bastola moja yenye risasi 11 na fedha bandia shilingi milioni 1.18, ambazo huzitumia kama geresha kuwa wanataka kuweka fedha kisha kumvamia wakala kwa kumtolea bastola.

“Hiyo bastola ina uwezo wa kutunza rasasi 25 ila tulikuta 11 maana yake 14 zilituma na risasi 14 kwa maisha ya watu ni nyingi sana,” amesema Muliro.

Muliro amesema si dhamira ya Jeshi la Polisi kuwaua wahalifu lakini nao hawako tayari kupoteza askari wao hata mmoja hivyo ni lazima wajihami kwa mujibu wa sheria.

Comments are closed