Lissu Vs Jamhuri ngoma bado nzito, atumia saa nne kuwasilisha hoja za pingamizi
Katika uwasilishaji wa hoja zake hii leo Lissu alitoa hoja nzito akieleza kuwepo kwa tofauti kubwa kati ya rekodi mbili za kesi zinazotoka kwenye Mahakama tofauti moja kutoka Mahakama ya Kisutu ambayo nakala yake alipelekewa gereani Ukonga na nyingine kutoka Mahakama Kuu ambayo aliipata jana akiwa mahakamani hapo.