Kenya: Kilio zaidi huku bei ya petroli, dizeli na mafuta taa ikipanda kwa Ksh.9 kwa lita
Mamlaka ya udhibiti wa nishati na petroli (EPRA) Jumanne ilitangaza kupanda kwa bei ya mafuta kwa KSh9 kwa lita.
Mamlaka ya udhibiti wa nishati na petroli (EPRA) Jumanne ilitangaza kupanda kwa bei ya mafuta kwa KSh9 kwa lita.
Uhaba huo ulianza wiki iliyopita magharibi mwa Kenya kufuatia mzozo kati ya makampuni ya uuzaji wa mafuta na serikali kuhusu malipo ya ruzuku, duru zilisema.
Katika taarifa ya EPRA ya 14 Septemba lita ya petroli imeongezeka kwa Ksh. 7.58 na itauzwa kwa Ksh.134.72, lita ya dizeli imeongezeka kwa Ksh. 7.94 na itauzwa kwa 115.60 na mafuta ya taa yamepanda kwa Ksh. 12.97 na yatauzwa kwa Ksh. 110.82, bei hizi zikiwa kwa jiji la Nairobi.