Majaliwa atoa maagizo kwa TANROADS kuhusu ukarabati wa madaraja
Ametoa agizo hilo leo Jumatano (Aprili 16, 2025) alipokagua maendeleo ya ukarabati wa madaraja katika maeneo ya Matandu na Somanga Mtama, Wilaya Kilwa Mkoani Lindi kwenye barabara kuu ya Dar es Salaam – Lindi yaliyokuwa yamekatika kufuatia mvua zinazonyesha nchini.