Viongozi wa Afrika Mashariki wakubaliana kuwepo kwa jeshi la kikanda DR Congo
Viongozi wa Afrika Mashariki walikubaliana Jumatatu kutuma kikosi cha kikanda kujaribu kumaliza mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kutoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano.