WHO yatoa tahadhari juu ya uhaba wa chanjo ya Kipindupindu
Tahadhari hiyo imetolewa katika wakati ambapo dunia inakabiliwa na uhaba wa chanjo dhidi ya ugonjwa huo wa kuharisha.
Tahadhari hiyo imetolewa katika wakati ambapo dunia inakabiliwa na uhaba wa chanjo dhidi ya ugonjwa huo wa kuharisha.
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia wafanyabiashara wa madini 10 kwa tuhuma za utoroshaji wa madini Kilogramu 9.8yenye thamani ya Tsh 1,555,476,586
Wanasayansi wanasema wamefanikiwa kuondoa kabisa virusi vinavyosababisha Ukimwi (VVU) kutoka kwenye seli za mwili zilizoambukizwa, kwa kutumia teknolojia ya kurekebisha upya jeni za mwili ya Crispr (Crispr gene-editing technology) iliyoshinda Tuzo ya Nobel
Rais Samia Suluhu Hassan alishika hatamu ya nchi kufuatia kifo cha mtangulizi wake huyo hivyo kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza taifa hilo tangu lipate uhuru.
Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kutekeleza ahadi yake ya kutunga sheria ya kuiwezesha Tume Huru ya Uchaguzi kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Taarifa ya TBS iliyotolewa kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa chakula hicho kilipoingizwa nchini kilifanyiwa ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara na kuthibitishwa kuwa ni salama kwa matumizi.
Hata hivyo anakiri kwamba kulikuwa na ugumu uliosababisha kuchukua saa 48 kabla ya rais mwingine hajaapishwa jambo ambalo ni kinyume na Katiba ya Tanzania, hali iliyotokana na pande mbili kuwa kutofautiana kimaamuzi.
Serikali imewasilisha mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2024/25. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo aliwasilisha mpango huo Dodoma jana katika kikao cha kamati ya bunge zima kilichoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana kilitangaza awamu nyingine ya maandamano yenye utofauti na awamu ya kwanza ya maandamano iliyomalizika hivi karibuni.
Wakazi saba wa Jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mbele ya mahakimu watatu tofauti wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka manne yakiwamo ya kusafirisha sukari na mafuta ya kupikia kwa magendo vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 10.7.