Wakili wa kujitegemea Peter Madeleka ashikiliwa na Polisi Arusha.
Madeleka kabla ya kukamatwa alilazimika kung’ang’ania kwa zaidi ya Dakika 30 katika chumba cha Mahakama (chember court) cha Jaji Aisha Bade ambaye awali ndiye alitoa maamuzi katika kesi yake ya kupinga makubaliano ya kukiri kosa.