Serikali ya Tanzania yakosoa makala ya BBC kuhusu Tundu Lissu
Serikali ya Tanzania imeikosoa makala iliyochapishwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kupitia kipindi chake cha BBC Africa Eye, ikidai kuwa imewasilisha taarifa zisizo na uwiano kuhusu kesi inayomkabili kiongozi wa upinzani, Tundu Lissu.