Ghasia zaibuka Nairobi: Kifo cha Mwalimu mikononi mwa Polisi chazua hasira mpya
Jeshi la polisi nchini Kenya limetumia mabomu ya machozi leo Alhamisi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakilaani mauaji ya mwalimu mmoja aliyefariki akiwa chini ya ulinzi wa polisi, hali iliyotishia kufunika juhudi za serikali kuwasilisha bajeti mpya bila kuchochea ghasia kama za mwaka uliopita.