UN imesema dola bilioni 1.7 zinahitajika kuisaidia Ukraine.
Hii ni kufuatia kuongezeka kwa mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine yaliyosababisha mahitaji makubwa ya kibinadamu baada ya huduma muhimu kuathirika na maelfu ya watu kufungasha virago kuzikimbia nyumba zao kwenda kusaka usalama.