Search
Close this search box.
Europe

Ukraine yakaidi masharti ya Urusi ya kusalimu amri katika mji wa Mariupol

18

Maafisa wa Ukraine wamekaidi masharti ya Urusi ya kuwataka wanajeshi wa Ukraine walioko katika mji uliozingirwa wa Mariupol waweke chini silaha zao na kusalimu amri, ili wapewe njia salama ya kuondoka katika mji huo wa kimkakati. 

Urusi imekuwa ikiushambulia kwa mabomu mji huo ulio kwenye bahari ya Azov, ikiilenga shule ya sanaa inayowapa hifadhi watu 400, saa chache kabla ya kuahidi kufungua njia mbili kwa wanajeshi wa Ukraine kuondoka. 

Urusi ilikuwa imeipa Ukraine hadi saa kumi na moja alfajir ya leo kuwa imesalimu amri mjini Mariupol, lakini haikusema itafanya nini ikiwa Ukraine itakataa kuheshimu matakwa yake.

Mzozo wa Ukraine na Urusi unazidi kuchukua sura mpya tangu Urusi iivamie Ukraine Februari mwaka huu, licha ya matammko ya kuitaka Urusi kusitisha mapigano bila masharti yeyote kutolewa.

Mapema hii leo Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell, amelaani shambulio la Urusi kwenye mji wa bandari wa Mariupol wa Ukraine kwamba ni Borrell amesema hayo wakati umoja huo ukijadili kuiwekea Moscow vikwazo zaidi.

Related Tags:

Comments are closed

Related Posts