MICHEZO YA PARALYMPICS TOKYO

Mataifa 163 yanashiriki michezo ya Paralympics mwaka huu huku wanariadha 4,400 wakishiriki katika michezo 22.

0
TOKYO PARALYMPICS 2020

Ufunguzi rasmi wa michezo ya Olimpiki kwa walemavu Paralympics, ulifanyika 24 Agosti 2021, bendera ya Afghanistan ikitumika kama ishara ya mshikamano na amani. Michezo ya Paralympics inafanyika kati ya Agosti 24 hadi 5 Septemba 2021.Mataifa 163 yanashiriki michezo ya mwaka huu huku wanariadha 4,400 wakishiriki katika michezo 22. Kati ya timu zinazoshiriki michezo hiyo ni timu ya wakimbizi inayoshirikisha watu 6 kutoka mataifa tofauti.Timu ya Wakimbizi inajumuisha wanaume watano na mwanamke mmoja watakaokuwa wakishindana katika michezo ya taekwondo na kuogelea.

Michezo Paralympics

Kati ya wanariadha wa timu ya wakimbizi ni Mohammed Abbas Karimi. Karimi ni mkimbizi kutoka Afghanistan na alizaliwa bila mikono. Mwaka wa 2017, Karimi (24) alishiriki katika michezo ya walemavu ya World Para Swimming Championships na kujishindia medali ya fedha, aliteuliwa na Shirika la UNHCR kuwa mjumbe maalum wa shirika hilo. Mohammed Karimi anatarajia kufanya vyema katika mashindano ya mwaka huu.

Mohammed Abbas Karimi

Baadhi ya mataifa ya Afrika yanayoshiriki Paralympics ni Kenya,Afrika Kusini,Malawi, Uganda na Tanzania.

Mataifa tofauti Paralympics

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted