Ethiopia yasheherekea mwaka mpya 2014

Sikukuu ya mwaka mpya nchini Ethiopia inasheherekewa 11 Septemba,ikijulikana kama Enkutatash,katika lugha ya Amharic, lugha rasmi ya Ethiopia. Sikukuu hii ikiwa ni ya kusheherekea siku ya kwanza ya...

0

Sikukuu ya mwaka mpya nchini Ethiopia inasheherekewa 11 Septemba,ikijulikana kama Enkutatash,katika lugha ya Amharic, lugha rasmi ya Ethiopia. Sikukuu hii ikiwa ni ya kusheherekea siku ya kwanza ya mwaka ya Meskerem, kulingana na kalenda ya Ethiopia.

Nchi ya Ethiopia ni kati ya mataifa mengine kama vile Eritrea, Afganistan,Iran na Nepal ambayo hayatumii kalenda inatumiwa na mataifa mengi ya Gregorian. Kalenda ya Gregorian inategemea kipindi ambacho dunia inazunguka jua ikiwa na siku 365 na miezi 12 kwa mwaka.

Taifa la Ethiopia linatumia kalenda iliyotofauti sana na ya mataifa mengine, ikiwa imejumuisha kalenda ya Julian na ile ya Misri na inategema kipindi ambacho dunia inazunguka jua.Kalenda hiyo ilianzishwa na kanisa la Roma mwaka wa 525 AD.

Kalenda ya Ethiopia kwa sasa iko miaka saba na miezi nane nyuma ya kalenda ya Gregorian, ikiwa na miezi 13 kwa jumla,miezi 12 ya kwanza ina siku 30 na mwezi wa 13 unaojulikana kama Pagume una siku 5 au 6 iwapo ni mwaka mrefu, kwa hiyo
Jumamosi 11 ni mwanzo wa mwaka wa 2014.

Sherehe za mwaka mpya zinajulikana kama ‘Enkutatash’ jina hilo likimaanisha ‘zawadi ya vito’ ikiwa kumbukumbu ya siku Malkia wa Sheba aliporudi Ethiopia baada ya kumtembelea Mfalme Solomon mjini Jerusalem mwaka 980 BC. Jina ‘enku’ pia likimaanisha mashambani ambako maua aina ya Adey Abeba,humea kwa wingi mwishoni mwa msimu wa mvua,maua hayo ya manjano yakiashiria mwanzo wa mavuno.

Sherehe za Mwaka Mpya wa Ethiopia kawaida hudumu kwa wiki moja na huzingatia hafla za kifamilia.

‘Enkuan Aderesachihu!’ Sherehe njema za mwaka mpya.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted