Mapinduzi ya serikali za mataifa ya Afrika

Kutoka Afrika magharibi, Burkina Faso imekuwa na mapinduzi mengi yaliyofaulu. Serikali za Burkina Faso zimepinduliwa mara saba na jaribio moja ambalo halikufaulu.

0

Mapinduzi yanayoongozwa na jeshi yamekuwa kama jambo la kawaida Afrika kufuatia mapinduzi kadhaa ambayo yamefanyika katika miaka ya hivi karibuni.

Kati ya mapinduzi ya hivi karibuni ni pamoja na yale ya Guinea yaliyoongozwa na Luteni Kanali Mamady Doumbouya 5 Septemba nchini Guinea yaliyomuondoa madarakani Rais Alpha Conde.

Luteni Kanali Mamady Doumbouya

Mapinduzi mengine yaliyofanyika hivi karibuni ni yale ya Mali.Mapinduzi nchini Mali yalianza usiku wa 24 Mei 2021, wakati jeshi lililongozwa na Makamu Rais Assimi Goita yalipomkamata Rais Bah N’daw, Waziri Mkuu Moctar Ouane na Waziri wa Ulinzi
Souleymane Doucoure. Assimi Goita, mkuu wa junta aliongoza mapinduzi hayo na kutangaza kuwa N’daw na Ouane wamevuliwa madaraka na kuwa uchaguzi utafanywa 2022.

Mapinduzi ya Mali ni ya tatu katika kipindi cha miaka 10 kufuatia jeshi kuchukua
uongozi 2012 na 2020.

Sudan imekuwa na majaribio 15 ya mapinduzi na 5 kati yao yalifaulu. Mapinduzi ya hivi karibuni yalikuwa ya mwaka 2019 yaliyomuondoa Omar al Bashir uongozini. Rais Bashir pia aliingia uongozini baada ya kuongoza mapinduzi mwaka wa 1989 na
akawa Rais wa Sudan kwa miaka 25.

Omar al Bashir, Rais wa zamani Sudan

Kutoka Afrika magharibi, Burkina Faso imekuwa na mapinduzi mengi yaliyofaulu. Serikali za Burkina Faso zimepinduliwa mara saba na jaribio moja ambalo halikufaulu.

Burkina Faso ilipata uhuru wake kutoka Ufaransa mwaka wa 1960 na Maurice Yameogo akawa rais wa kwanza. Baada ya maandamano ya wanafunzi na wanachama wa vyama vya wafanyakazi, Rais Yameogo alipinduliwa na Sangoule Lamizana mwaka wa 1966 na Lamizana akawa rais. Njaa kali pamoja na matatizo kutoka kwa vyama vya wafanyakazi nchini yalichangia kupinduliwa kwa serikali ya Rais Lamizana mwaka wa 1980, mapinduzi hayo yaliongozwa na Saye Zerbo, aliyechukua hatamu za uongozi.

Rais Saye Zerbo pia alikumbana na matatizo na upinzani kutoka kwa vyama vya wafanyikazi, nae pia akapinduliwa mwaka wa 1982, mapinduzi hayo yaliongozwa na Jean- Baptiste Ouedraogo.Thomas Sankara alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu, ila baadae akazuiliwa jela. Shinikizo la kutaka kuachiliwa kwa Thomas Sankara kulichangia mapinduzi ya 1983 na Thomas Sankara akawa Rais.

Rais Thomas Sankara alipinduliwa mwaka wa 1987 katika mapinduzi yaliyoongozwa na Blaise Campaore. Blaise Campaore akawa rais na hata baada ya majaribio ya mapinduzi ya 1989,ameshinda uchaguzi wa 1991 na 1998.

Blaise Campaore

Mataifa mengine ambako kumekuwepo na mapinduzi na majaribio ya mapinduzi ni pamoja na mataifa ya Burundi, Sierra Leone, Ghana, Uganda na Kenya.

Burundi imekuwa na mapinduzi 11 yakichangiwa na vita vya kimbari kati ya jamii za Hutu na Tutsi. Sierra Leone imekuwa na mapinduzi matatu kati ya mwaka wa 1967 na 1968 na majaribio ya mapinduzi mwaka wa 1971. Kati ya 1992 na 1997 kulikuwa na majaribio matano ya mapinduzi. Taifa la Ghana limekuwa na mapinduzi nane katika
kipindi cha miongo miwili.

Nchini Kenya kulikuwa na jaribio la mapinduzi mwaka 1982 yakumng’oa madarakani Rais wa pili wa Kenya Daniel Arap Moi. Usiku wa kuamkia 1 Agosti majeshi ya Kenya Airforce yaliteka kambi ya majeshi ya Eastleigh viungani mwa Nairobi, na kituo cha redio cha VOK na kutangaza kuwa jeshi limechukua uongozi wa serikali. Jaribio hilo la mapinduzi halikufaulu na walioongoza mapinduzi hayo walikamatwa na kupewa hukumu ya kifo.

Katika uchaguzi uliofanywa nchini Uganda mwaka wa 1980,chama cha Yoweri Museveni cha Uganda Patriotic Movement (UPM) kilishindwa na kile cha Milton Obote cha Uganda People’s Congress (UPC). Milton Obote akaapishwa kuwa rais, Yoweri Museveni alidai
kulikuwa na wizi wa kura na akaanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka wa 1981. Mwaka wa 1985 Jenerali Tito Okello alimuondoa Milton Obote uongozini na kuchukua hatamu za uongozi. Januari mwaka wa 1986,Yoweri Museveni alimpindua Okello na akawa rais.

Rais Yoweri Museveni

Rais Yoweri Museveni amekuwa uongozini nchini Uganda kutoka mwaka 1986 alipompindua Jenerali Tito Okello.

Kwa ujumla Afrika imekuwa na mapinduzi mengi ikitofautishwa na mabara
mengine.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted