Jaribio la mapinduzi latibuliwa Sudan

Takriban maafisa 40 wa jeshi wanaodaiwa kuhusika na jaribio hilo la mapinduzi wamekamatwa.

0

Kumekuwa na jaribio la mapinduzi Sudan Jumanne 21. Kulingana na ripoti za vyombo vya habari nchini humo, wandani wa aliyekuwa rais wa Sudan Omar al Bashir walihusika na jaribio hilo la Jumanne asubuhi.

Inasemekana kuwa kulikuwa pia na jaribio la kukiteka kituo cha redio cha Omdurman kilichoko karibu na mji mkuu Khartoum.Takriban maafisa 40 wa jeshi wanaodaiwa kuhusika na jaribio hilo la mapinduzi wamekamatwa, kufuatia jaribio hilo majeshi ya Sudan yamepelekwa mji mkuu Khartoum kutuliza hali.

Jaribio hili la mapinduzi limefanyika wakati Sudan inapanga kufanya mabadiliko ya katiba na kufanya uchaguzi mkuu. Shuhuda mmoja mjini Khartoum anasema kuwa majeshi wametumia magari ya kijeshi kuziba daraja inayounganisha Khartoum na
Omdurman mapema Jumanne 21.

Sudan inaoongozwa na serikali ya umoja kati ya jeshi na raia baada ya kupinduliwa kwa rais wa zamani Omar al-Bashir mwezi Aprili 2019.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted