Kuosha vyoo vya wanawake ndio kazi pekee wanawake wa Afghan wanaruhusiwa kufanya.

Kazi ambazo wanawake Afghanistan wanaruhusiwa kufanya pekee ni zile ambazo wanaume hawawezi kufanya, kama kusafisha vyoo vya wanawake. Wafanyakazi wanawake waliokuwa wakifanya kazi katika serikali ya mji wa...

0

Kazi ambazo wanawake Afghanistan wanaruhusiwa kufanya pekee ni zile ambazo wanaume hawawezi kufanya, kama kusafisha vyoo vya wanawake.

Wafanyakazi wanawake waliokuwa wakifanya kazi katika serikali ya mji wa Kabul wameambiwa wasiende kazini tena, wanawake watakaoruhusiwa kufanya kazi ni wale ambao kazi zao haziwezi kufanywa na wanaume, hivi vikiwa vikwazo vya hivi karibuni vilivyowekwa na Taliban nchini Afghanistan.

Amri hiyo,imetangazwa na kaimu Meya wa Kabul Hamdullah Nohmani Jumapili 19. Amri hiyo inamaanisha kuwa wanawake hawaruhusiwi kufanya kazi katika serikali ya mji mkuu wa Kabul.Moja ya kazi ambazo wanawake wanaweza kufanya katika serikali ya Kabul ni kusafisha vyoo vya wanawake, tangazo hilo limetaja.

Amri hiyo inawaacha wanawake wengi bila kazi. Nohmani amesema kuna takriban watu 2,930 wanaofanya kazi kwenye manispaa na 27% ya hao ni wanawake.

Hofu inazidi kuongezeka kati ya wanawake na wasichana nchini Afghanistan baada ya Taliban kuchukua uongozi wa nchi hiyo mwezi Agosti. Licha ya hakikisho la mara kwa mara la kuheshimu haki za wanawake, amri hii mpya kwa wafanyakazi wanawake ni
ishara ya hivi punde ya ukiukaji wa haki za wanawake baada ya Taliban kurudi madarakani baada ya miaka 20.

Hamdullah Nohmani, kaimu Meya wa Kabul

Tangu Taliban walipochukua uongozi, wanawake wameamriwa kuacha kazi na wanafunzi wa kike hawaruhusiwi kuenda shule, nwanawake waliokuwa wameshikilia nyadhfa za uongozi wameondolewa kutoka nyadhfa hizo.

Mara ya mwisho Taliban walipokuwa uongozini kati ya 1996 na 2001, kundi hilo liliwawekea marufuku wanawake na wasichana kuenda kazini na shule, hawakuruhusiwa kutoka nyumbani pekee yao na walilazimshwa kujifunika mwili mzima.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted