Taliban yatoa marufuku wanaume kunyoa ndevu.

Taliban yapiga marufuku vinyozi kuwanyoa wanaume vichwa na ndevu, wakisema kunyoa kunakwenda kinyume na maadili ya dini ya kiislamu.

0

Taliban imepiga marufuku vinyozi katika mkoa wa Helmand kuwanyoa wanaume vichwa na ndevu, wakisema kunyoa kunakwenda kinyume na maadili ya dini ya kiislamu. Mtu yeyote atakaye kwenda kinyume na sheria hiyo mpya atachukuliwa hatua,polisi wa Taliban wamesema.Vinyozi kutoka mji mkuu wa Kabul wanasema pia wamepata masharti hayo.

Masharti haya mapya yanadhihirisha kurudi kwa uongozi wa sheria kali wa Taliban licha ya kuahidi mfumo tofauti wa uongozi.

Tangu Taliban ichukue uongozi mwezi jana, wamewaadhibu vikali wapinzani wao. Jumamosi 25 Septemba,waliwaua watu wanne kwa madai ya utekajinyara, miili ya wanne hao ilining’inizwa katika barabara za mji wa Herat.

Katika ilani iliyobandikwa kwenye vinyozi kusini mwa mkoa wa Helmand, maafisa wa Taliban waliwaonya vinyozi kufuata sheria za kiislamu za Sharia katika kuwanyoa wanaume nywele na ndevu.

“Hakuna mtu yeyote aliye na haki ya kulalamika”ilani hiyo ilisema

Wakati wa uongozi wa Taliban kati ya 1996 hadi 2001, walipiga marufuku mitindo tofauti ya nywele na kusisitiza kuwa wanaume wanastahili kukuza ndevu zao.Tangu hapo wanaume wa Afghan wamekuwa wakinyoa mitindo tofauti ya kisasa.

Tangu sheria hii mpya iwekwe, vinyozi wengi wanalalamika kuwa biashara imekuwa ngumu kwao na wanapata hasara kubwa.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted