Utajiri wa mwanzilishi wa Facebook ulivyoporomoka kwa saa chache.

Utajiri wa mwanzilishi wa Facebook ulivyoporomoka kwa saa chache.

0
Mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg

Huduma za mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp na Instagram hapo jana zilipotea kwa takribani saa nane, huku sababu ya kutoweka kwa mitandao hiyo zikitajwa kuwa ni mifumo ya uendeshaji kupata hitilafu kubwa zaidi kuwahi kutokea.

Huduma zote tatu zinamilikiwa na Facebook, na hazikuweza kupatikana kwenye wavuti au kwenye programu za simu za mkononi.

Kupotea kwa huduma hizo kwa muda huo kumesababisha utajiri wa Mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg kuanguka kwa wastani wa dola bilioni 5.9, kwenye saa ambazo Facebook, Instagram na WhatsApp hazikua zinafanya kazi.

 Kwa sasa Mark anashikilia namba  6 kwenye orodha ya Matajiri Duniani kote  akiwa na utajiri wa dola bilioni 116.

Taarifa iliyotumwa usiku wa kuamkia leo Oktoba 5, 2021 imesema mabadiliko mabaya ya usanifu yaliathiri zana na mifumo ya ndani ya kampuni hiyo.

Facebook imesisitiza kwa kuwatoa wasiwasi watumiaji wake kuwa kilichotokea ni tatizo la ndani na si udukuzi.

Usumbufu huo unakuja siku moja baada ya mahojiano na mfanyakazi wa zamani wa Facebook ambaye alivujisha nyaraka kuhusu kampuni hiyo

Mitandao hiyo yote kwa sasa inafanya kazi kama kawaida.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted