Nchi ya Tonga yaripoti kisa cha kwanza cha UVIKO 19.

Ripoti ya UN tarehe 29 Oktoba 2021 imeonyesha kuwa mataifa manne pekee hayajaripoti visa vyovyote vya UVIKO 19.

0

Nchi ya kisiwa ya Tonga imeripoti kisa chake cha kwanza cha UVIKO 19 tangu ugonjwa huo ulipolipuka mapema mwaka 2020 nchini China. Kisa hicho kimeripotiwa kwa mtu aliyewasili nchini humo kutoka New Zealand.

Katika taarifa yake kwa taifa Waziri Mkuu wa Tonga Pohiva Tu’i’onetoa alithibitisha kisa kimoja kati ya wasafiri 215 waliowasili kutoka mji wa Christchurch New Zealand.

Tonga ni nchi ilioko kaskazini mashariki mwa New Zealand, na idadi ya watu 106,000 pekee. Kulingana na utafiti wa Our World Group, takriban 31% ya raia wa Tonga wachanjwa kikamilifu na 48% wamepata angalau chanjo ya kwanza.

Tonga ni kati ya mataifa machache duniani yaliyoweza kuepuka kabisa ugonjwa wa UVIKO 19. Mataifa jirani na Tonga kama vile Fiji pia iliweza kuepuka ugonjwa huo kwa muda mrefu hadi mwaka huu mwezi Aprili ambapo kirusi cha Delta kilipoathiri nchi hiyo ua kisiwa na kuwaambukiza zaidi ya watu 50,000 na kuwaua wengine 673.

Tonga

Tangu kulipuka kwa UVIKO 19, ugonjwa huo umesambaa katika mataifa mengi na kuwaua mamilioni ya watu, ila kuna mataifa mengine ambayo hadi sasa hayajaripoti visa vyovyote, hayo ikiwa ni kulingana na Shirika la Afya Duniani WHO.

Kulingana na utafiti, visa zaidi ya milioni 240 vimeripotiwa na vifo zaidi ya milioni 5 kuripotiwa, vingi ya vifo hivyo vikitokana na kuenea kwa kirusi cha Delta.

Mengi ya mataifa yaliyofaulu kuepuka UVIKO 19 ni mataifa ya visiwa katika bahari za Atlantic na Pacific.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya tarehe 29 Oktoba 2021 imeonyesha kuwa mataifa manne pekee hayajaripoti visa vyovyote vya UVIKO 19, ikiwa ni Turkmenistan,Korea Kaskazini, Tuvalu na Nauru.

Nchi hizi zimefaulu kuepuka ugonjwa wa UVIKO 19 kutokana na kuwa ni mataifa ya visiwa na pia kuweka mikakati madhubuti ya kuepuka ugonjwa huo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted