Somalia: Mlipuko wa bomu mjini Mogadishu wasababisha maafa na uharibifu

Watu watano wameuawa na wengine zaidi kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu kwenye gari mjini Mogadishu siku ya Alhamisi,

0

Watu watano wameuawa na wengine zaidi kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu kwenye gari karibu na shule katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu siku ya Alhamisi, afisa wa usalama alisema, katika shambulio la hivi punde kuikumba nchi hiyo.

Inadaiwa kuwa mlipuko huo uliotokea katika makutano ya K4 ulikuwa unalenga msafara wa Muungano wa Afrika. Idadi ya wale waliouawa ikiwa imeongezeka hadi watu wanane.

“Kulikuwa na mlipuko wa bomu kwenye gari… vifo vya watu watano vilithibitishwa na wengine 15 kujeruhiwa,” afisa wa usalama Mohamed Abdillahi alisema na kuongeza kuwa wanafunzi 11 ni miongoni mwa wale waliojeruhiwa.

“Hatujui lengo la shambulio hilo… (lakini) kulikuwa na gari la kibinafsi la lililopita eneo hilo,” aliongeza.

Mkurugenzi wa huduma ya ambalanzi Aamin ya Mogadishu, Abdikadir Abdirahman, alichapisha picha za athari za mlipuko huo kwenye Twitter, akiita mlipuko huo “janga”.

Hakukuwa na madai ya mara moja ya nani alihusika na mlipuko huo, lakini kundi la wanajihadi la Al-Shabaab limedai mashambulio mengine ya mabomu mjini Mogadishu, likiwemo shambulio baya la Jumamosi ambalo lilimuua mwandishi wa habari maarufu wa Somalia.

Abdiaziz Mohamud Guled, mkurugenzi wa Radio Mogadishu inayomilikiwa na serikali, alikuwa mkosoaji mkali wa wanamgambo wanaohusishwa na Al-Qaeda.

Al-Shabaab, ambayo imekuwa ikiendesha uasi mkali dhidi ya serikali dhaifu ya nchi hiyo tangu 2007, ilidai kuhusika na shambulio la bomu la kujitoa mhanga katika taarifa yao ilisema wapiganaji wake walikuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu mwandishi huyo.

Al-Shabaab waliudhibiti mji mkuu hadi mwaka 2011 walipofukuzwa na wanajeshi wa Umoja wa Afrika, lakini bado wanashikilia maeneo ya mashambani na wamekuwa wakiendeleza mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya  serikali na raia mjini Mogadishu na kwingineko.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted