Watu sita wafariki kwenye mafuriko Afrika Kusini

Mvua za ghafla zimenyesha sehemu za mkoa wa kusini ikijumuisha East London kwenye pwani ya Bahari ya Hindi

0

Takriban watu sita, akiwemo mpigambizi wamefariki katika mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa inayonyesha katika jimbo la Eastern Cape nchini Afrika Kusini, afisa mkuu wa kanda alisema Jumapili.

“Jumla ya watu sita walifariki katika matukio tofauti ikiwa ni pamoja na mhudumu wa… polisi,” Oscar Mabuyane, Mkuu wa Mkoa wa Cape Mashariki alisema katika taarifa yake, akisasisha idadi ya waliofariki.

Polisi huyo alifariki akiendeleza shughuli za uokoaji

Mvua za ghafla zimenyesha sehemu za mkoa wa kusini ikijumuisha East London kwenye pwani ya Bahari ya Hindi, Jumamosi.

Ndani ya saa chache, maeneo ya mabondeni yalikuwa yamefurika kwa kiasi kikubwa, afisa wa serikali ya eneo hilo aliambia AFP.

Miongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni Mdantsane, kitongoji kinachokua karibu na East London.

Idadi kubwa ya watu hasa kutoka Mdantsane wameyakimbia makazi yao na baadhi ya barabara “zimezibwa kutokana na mafuriko na kutatiza juhudi za kufikia jamii katika maeneo hayo,” ilisema taarifa hiyo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted