AFCON: Msongamano uwanjani wasababisha vifo vya watu wanane

Wanawake wawili wa miaka thelathini, wanaume wanne wenye umri wa miaka thelathini, mtoto mmoja, waliuawawa katika msongamano huo

0
Mashabiki wa Gambia uwanjani Cameroon (Photo by Pius Utomi EKPEI / AFP)

Watu wanane wameuawa na wengine takriban 50 kujeruhiwa katika msongamano uliotokea katika uwanja wa michezo katika mji mkuu wa Cameroon Yaounde kabla ya mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika siku ya Jumatatu, televisheni ya taifa iliripoti.

Wanawake wawili wa miaka thelathini, wanaume wanne wenye umri wa miaka thelathini, mtoto mmoja, waliuawawa katika msongamano huo ripoti hiyo ilisema. Habari za serikali ziliripoti hapo awali kwamba watu sita walikuwa wameuawa na kadhaa kujeruhiwa.

“Mshindo mkubwa kwenye lango la Uwanja wa Olembe,” ulisababisha “ vifo vya watu kadhaa na wengine kujaruhiwa” kulingana na shirika la utangazaji la serikali ya Cameroon CRTV.

Shirikisho la Soka barani Afrika, ambalo huandaa mchezo huo barani lilisema linafahamu kuhusu tukio hilo.

Katika taarifa iliyotumwa mtandaoni CAF ilisema “inachunguza hali hiyo na kujaribu kupata maelezo zaidi juu ya kile kilichotokea.”

Shirikisho hilo lilisema limemtuma katibu mkuu wake “kuwatembelea mashabiki waliojeruhiwa katika hospitali ya Yaounde” na kuongeza kuwa ilikuwa na “mawasiliano ya mara kwa mara na serikali ya Cameroon na Kamati ya Maandalizi ya nchini humo.”

Dakika chache baada ya kipenga cha mwisho cha mechi kati ya Cameroon na Comoro hakukuwa na athari ya mkanyagano uwanjani, alibainisha mwandishi wa habari wa AFP.

Cameroon ilishinda mechi hiyo kwa mabao 2-1.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted