Amerika: Mtoto wa umri wa miaka 4 ajipiga risasi mamake akijivinjari

Mamake mtoto alikuwa amekiti kiti cha mbele cha gari na mtoto wake kiti cha nyuma alipojipiga risasi

0

Mtoto wa umri wa miaka minne kwa jina Jarrion Walker kutoka nchini Amerika,alijipiga risasi na kufariki akiwa kwenye gari.

Kulingana na polisi wa mji wa Jefferson Parish katika jimbo la Louisiana, mtoto huyo alitumia bastola ya mzazi wake na kujipiga risasi akiwa ameketi kiti cha nyuma cha gari na mamake akiwa amekiti kiti cha mbele na mpenziwe.

Mamake mtoto huyo alikuwa akivuta bangi na mpenziwe katika kiti cha mbele cha gari hilo na anasema hakumuona mtoto huyo akichukua bastola.

Tukio hilo lilifanyika Jumamosi mwezi Januari mwendo wa saa tano kasorobo, mtoto huyo Jarrion akiwa amekaa katika kiti cha nyuma na ndugu zake wadogo mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja na mwingine wa miezi 22.

Afisa mkuu wa polisi kutoka Jefferson Parish Joe Lopinto anaamini kwamba mtoto huyo alijipiga risasi kwa bahati mbaya. Alifariki hospitalini alikopelekwa.

Wakati huo huo, mamlaka inasema mama huyo na mpenzi wake wanashirikiana na polisi lakini bado hawajafunguliwa mashtaka ya uhalifu.

“Bastola zinapaswa kufungiwa” Sheriff Lopinto alisema katika mahojiano na chanzo cha habari Jumapili usiku.

“Madhara mabaya yanaweza kutokea iwapo silaha hizi hazitawekwa mbali na watoto,” aliongeza.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted