Habari njema, maambukizi mapya ya UVIKO 19 yaanza kupungua duniani kote

Janga la UVIKO-19 limeanza kupungua kote duniani wiki hii baada ya miezi mitatu na nusu ya ongezeko la maambukizo.

0

Janga la UVIKO-19 limeanza kupungua kote duniani wiki hii baada ya miezi mitatu na nusu ya ongezeko la maambukizo.

Hivi ndivyo hali ilivyo kwa sasa

– visa vyapungua kwa 10%

Idadi ya visa vya UVIKO 19 vya kila siku duniani vilipungua kwa asilimia 10 wiki hii hadi milioni 3.03, baada ya kuongezeka kwa wiki 15 mfululizo, kulingana na hesabu ya AFP hadi Alhamisi.

Kesi zilizothibitishwa zinaonyesha sehemu ndogo tu ya idadi halisi ya maambukizo, na viwango vya upimaji katika nchi tofauti.

Takriban kila eneo la dunia llilionyesha kupungua kwa visa vya UVIKO 19 katika siku saba zilizopita

Katika nchi za Amerika na Canada idadi ya visa vipya vya kila siku ilipungua kwa asilimia 38, huku Afrika visa vikipungua kwa asilimia 21 na Asia ikapungua kwa asilimia 16.

Kesi katika eneo la Amerika ya Kusini/Caribbean zilipungua kwa asilimia 13 na Mashariki ya Kati kwa asilimia nne.

Hali ilikuwa karibu shwari barani Ulaya, na ongezeko la asilimia moja.

Idadi ya maambukizo katika mataifa ya Oceania ilipungua kwa karibu asilimia kumi.

– Ongezeko kubwa lipo katika mataifa ya

Iran ilishuhudia ongezeko kubwa zaidi katika idadi ya maambukizi mapya wiki hii ikiwa ni ongezeko la asilimia 233.

Visa vya UVIKO 19 katika Visiwa vya Solomon katika bahari ya Pasifiki vikiwa vimeongezeka kwa asilimia 138, Armenia ikiwa na asilimia 137, Azabajani ikiongezeka kwa asilimia 133, wakati visa vikiongezeka mara mbili huko Korea Kusini.

Nchi iliyoripoti visa vichache vya maambukizi

Jamhuri ya Dominica ilishuhudia upungufu mkubwa zaidi wa visa vya UVIKO 19 kwa wiki ikiwa visa hivyo vimepungua kwa asilimia 65, ikifuatiwa na Nepal iliyopungua kwa asilimia 55, Argentina (ikipungua kwa asilimia 51), Jamaica (ikipungua kwa asilimia 50) na Morocco (ikipungua kwa asilimia 49).

– Amerika ilikuwa na visa vingi vya UVIKO 19

Amerika ilibaki kuwa nchi iliyo na idadi kubwa zaidi ya visa vipya ikiwa ina rekodi visa 362,800 kwa siku, hata hivyo visa vikiwa vimeshuka kwa asilimia 39 katika wiki iliyopita.

Ufaransa imeripoti kushuka kwa maambukizi ikiwa na kesi 289,200 na India ambapo maambukizi yalipungua kwa theluthi hadi 204,500.

Kwa msingi, nchi iliyoripoti visa vipya zaidi kwa wiki ilikuwa Denmark yenye 5,337 kwa kila wakaazi 100,000, ikifuatiwa na Slovenia yenye 5,112, Israel (4,497), Georgia (3,508) na Ureno (3,455).

– Vifo vilivyoripotiwa

Idadi ya vifo vinavyotokana na UVIKO-19 iliongezeka duniani kote kwa wiki ya nne mfululizo hadi 10,507 kwa siku, ikiwa ni ongezeko la asilimia 16.

Ingawa kirusi cha Omicron kilisababisha maambukizo mara nne zaidi kwa kila siku kuliko mawimbi ya hapo awali, vifo vya kila siku vinasalia chini sana kuliko rekodi ya mapema Januari 2021 vilivyofika15,000.

Amerika ilirekodi vifo vingi zaidi wiki hii ikiwa ni vifo 2,576 kwa siku zaidi ya vile viliporitiwa India (1,040) na Brazil (702).

Nchi zilizoripoti viwango vya juu zaidi ya vifo kwa uwiano wa idadi ya watu ilikuwa katika mataifa ya Balkan — Bosnia (vifo 11 kwa kila wakaazi 100,000), Croatia (8.9), Macedonia Kaskazini (8.7), na Montenegro na Bulgaria (8.0 kila moja)

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted