Pakistan: Mama mjamzito apigiliwa msumari kichwani ili ajifungue mtoto wa kiume

Huko Asia Kusini, mara nyingi mvulana anaaminika kuwapa wazazi wake usaidizi wa kifedha zaidi kuliko binti.

0

Mwanamke mjamzito kutoka Pakistan alipigiliwa msumari kichwani na mganga ambaye alisema ingemhakikishia kujifungua mtoto wa kiume, daktari wake alisema Jumatano.

Waganga wa kiimani ambao desturi zao zimekita katika ngano za mafumbo za Kisufi, ni za kawaida kote nchini Pakistan licha ya kukataliwa na baadhi ya shule za Kiislamu.

Huko Asia Kusini, mara nyingi mvulana anaaminika kuwapa wazazi wake usaidizi wa kifedha zaidi kuliko binti.

Mwanamke huyo alifika katika hospitali ilioko mji wa kaskazini-magharibi wa Peshawar baada ya kujaribu kung’oa msumari huo mwenyewe, daktari Haider Khan alisema.

“Alikuwa na fahamu kabisa, lakini alikuwa ni mwenye maumivu makali,” alisema Khan, ambaye aliondoa msumari huo.

Mama huyo wa mabinti watatu alikuwa na mimba ya msichana mwingine, daktari aliongeza.

Picha ya X-ray ilionyesha msumari wa sentimita tano (inchi mbili) ulikuwa umetoboa sehemu ya juu ya paji la uso la mwanamke huyo lakini ukaukosa ubongo wake.

Khan alisema nyundo au kitu kingine kizito kilitumika kuugonga msumari huo kichwani.

Mwanamke huyo awali aliwaambia wahudumu wa hospitali kuwa alikuwa amepigilia msumari kichwani mwake mwenyewe kutokana na ushauri wa mganga huyo wa imani, kabla ya kusema kuwa mganga ndiye aliyemgongela msumari kichwani.

Polisi wa Peshawar wanajaribu kumsaka mwanamke huyo ili kumhoji.

“Tumekusanya picha za CCTV kutoka hospitalini na tunatumai kumfikia mwanamke huyo hivi karibuni,”mkuu wa polisi wa jiji hilo Abbas Ahsan aliambia AFP.

“Hivi karibuni tutamtia mikononi mganga huyo,” alisema.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted